Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Nasser Ash-Shammari ameeleza kuhusu mpango unaoandaliwa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) wa kujipenyeza kwenye maeneo matakatifu; na kwa niaba ya muqawama wa Kiislamu wa nchi hiyo akazitishia tawala zinazofadhili na kuunga mkono ugaidi wa kitakfiri kwamba, watavihamishia vita kwenye ardhi zao wenyewe.
Ash-Sammari ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya An-Nujabaa amekosoa udhaifu wa serikali wa kushindwa kuwadhibiti magaidi na akabaiisha kuwa, harakati ya An-Nujabaa ina taarifa zinazothibitisha kuwa, kundi la kigaidi la Daesh linajipanga tena upya.
Msemaji wa harakati ya An-Nujabaa nchini Iraq ameashiria pia njama za magaidi za kutaka kufika hadi Karbala kupitia jangwa la Al Anbar na akaeleza kwamba, mmoja wa wajitoamhanga wawili wa shambulio la siku ya Alkhamisi mjini Baghdad alitokea kwenye mpaka wa Syria na akajipenyeza ndani ya ardhi ya Iraq kupitia mahali na wakati vikosi vya nchi hiyo vilipokuwa vikipokezana lindo.
Nasser Ash-Shammari amesisitiza: "Usalama wa nchi na kulinda maisha ya raia wa Iraq ni mstari mwekundu kwetu; na makundi ya muqawama wa Kiislamu yatavihamishia vita kwenye ardhi ya watu wanaotaka kuiteketeza Iraq."
Miripuko miwili ya mabomu iliyotokana na shambulio la kigaidi ilitokea siku ya Alkhamisi iliyopita kwenye eneo la al-Babu-Sharqi na mzunguko wa At-T'airan katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambapo kwa mujibu wa taarifa za karibuni za wizara ya afya ya nchi hiyo 32 waliuawa na wengine 110 walijeruhiwa.
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh lilitangaza kuwa ndilo lililohusika na jinai hiyo ya kinyama...
342/